nitarejea

diamond platnumz

vipi mizigo umeshaweka tayari

sijechelewa nkaachwa na gari

basi jikaze usilie mpenzi

mi nitarudi niombee kwa mwenyezi

zile taabu na njaa msimu mzima mavuno hakuna

huwa nakosa raha pale mkikosa cha kutafuna

roho yangu inauma

sema ntafanya nini na pesa sina

nakuonea na huruma

bora niende mjini kusaka tumaa

kama watoto wakinililia waambie kesho nitarejea

wadanganye na vibagia

waambie pipi ntawaletea

kama watoto wakinililia waambie kesho nitarejea

nawe usichoke kuvumilia

na kila siku kuniombea

wanajua kwamba nafsi na roho vitakuwa na wasiwasi

ukumbuke na moyo utajawa na simanzi

ntakapokuwa nakwenda shambani afu niko peke yangu honey

ntapokuja kuwa na majirani ntaumia aaah

pale napotoka kisimani ama nipo na kuni kichwani

sina wakunitua nyumbani ntaliaa

maneno yako yananfanya nakosa raha na mawazo

hata mwenzako sijawahi kufika dar huu ndo mwanzo

vile nakwenda na sijui pa kukaaa wala mavazi ooh

we niombee niepushwe na balaa na maradhi ooh

kama watoto wakinililia waambie kesho nitarejea

wadanganye na vibagia

waambie pipi ntawaletea

kama watoto wakinililia waambie kesho nitarejea

nawe usichoke kuvumilia na kila siku kuniombea

unapokwenda kama ukifika salama

utukumbuke na sisi

usisahau kama mkeo na wana

umetuacha na dhiki

vile usijali ila naomba chunga sana

ogopa na marafiki

wakikulaghai hata kwa mbegu za mtama

waambie sidanganyiki

unapokwenda kama ukifika salama

utukumbuke na sisi

kumbuka mkeo na wana nyumbani

umetuacha na dhiki ooh

vile usijali ila naomba chunga sana

ogopa na marafiki

wakikulaghai hata kwa mbegu za mtama

waambie sidanganyiki

ntarejea mama

niombee nirude salama

ohhh watoto wadanganye

ihh

ohh

kama watoto wakinililia waambie kesho nitarejea

wadanganye na vibagia

waambie pipi ntawaletea

kama watoto wakinililia waambie kesho nitarejea

nawe usichoke kuvumilia

na kila siku kuniombea