wanasemaga mapenzi safari
unavyopita ndo jinsi unajongea
ila niendako ni mbali sijui ka ntafika sababu natembea
yakisifika nikakesha nangojea
akabariki jalali na nikawika muziki nikauotea
kumbe mapenzi hayataki haraka
ni kama tango natia tu chumyi
na kujitia kitandani mjuzi
badala ya mbwa nikafuga mbuzi
wivu ukanifanya nikagombana na marafiki
ugomvi na mamangu akiniambia siambiliki
moyo ukanambia nasibu sasa mapenzi basi
ila nang'ang'ania najaribu kuipinga nafsi
esma ananiambia mdogo wangu mapenzi basi
nikiumizwa na huyu kesho nna mwingine
haki ya mungu siyawezi sema
ila nimejifunza kesho nisiwaamini wacheza sinema
siwezi kumeza siwezi tema
ndio maana sikushanga ile ghafla
wanasema kitanda ukitandika sharti ukilalie
nikajitia ukamanda yatakwisha
ndo visa machozi me nilie
mwisho wa siku akaichomoa chali
niliyvo mjinga nikacheat aibu mpaka
moyo unanambia nasibu sasa mapenzi basi
ila nang'ang'ania najaribu kuipinga nafsi
lizer ananiambia simba mapenzi basi
nikiumizwa na huyu kesho nna mwingine